Home » , » Bado Lulu ‘anamchanganya’ Bahati kutoka Kenya

Bado Lulu ‘anamchanganya’ Bahati kutoka Kenya

TANGAZO
Kitendo cha Elizabeth Michael ‘Lulu’ kumuweka msanii Bahati kutokea Kenya hotelini kinyume na makubaliano yao, bado hakimtoki kichwani muimbaji huo wa gospel.

Kwa mujibu wa Bahari mwaka 2016 alikuja Tanzania kwa ajili ya kufanya video ya wimbo wake ‘Maria’ na alipanga kumtumia Lulu kama video vixen, hata hivyo mrembo huyo hakutokea katika kikao walichopanga kingefanyika hotelini.

Kwa sasa Bahati amerudi tena Tanzania kwa ajili ya kufanya kazi na msanii wa WCB, Mbosso, hata hivyo bado anakumbuka alichofanyiwa na Lulu.

“Ilikuwa meeting ya video vixen, kama alinifanyia hivyo je anayempenda inakuwaje?, na mimi nilikuwa nimeweka shilingi kidogo, naongea kwa uchungu,” amesema Bahati hapo jana mara alipowasili Bongo.

Soma Pia; Bahati asimulia kilichomtokea kwa Lulu

Hata hivyo baada ya kutompata Lulu, Bahati alikuja kufanya video hiyo na Jokate Mwegelo.

Kabla ya tukio hilo kutokea, hapo awali muimbaji huyo aliwahi kueleza hisia zake kwa Lulu kupitia vyombo vya habari kwa kueleza kuwa iwapo atampata mrembo huyo atakuwa ametulia kabisa.
TANGAZO
Share this article :

Post a Comment