
Kitendo cha Elizabeth Michael ‘Lulu’ kumuweka msanii Bahati kutokea
Kenya hotelini kinyume na makubaliano yao, bado hakimtoki kichwani
muimbaji huo wa gospel.
Kwa mujibu wa Bahari mwaka 2016 alikuja Tanzania kwa ajili ya kufanya
video ya wimbo wake ‘Maria’ na alipanga kumtumia Lulu kama video vixen,
hata hivyo mrembo huyo hakutokea katika kikao walichopanga kingefanyika
hotelini.
Kwa sasa Bahati amerudi tena Tanzania kwa ajili ya kufanya kazi na
msanii wa WCB, Mbosso, hata hivyo bado anakumbuka alichofanyiwa na Lulu.
“Ilikuwa meeting ya video vixen, kama alinifanyia hivyo je anaye